Serikali
imeahidi kumchukulia hatua Shilole kufuatia kusambaa kwa picha zake
chafu zilizopigwa wakati akitumbuiza nchini Ubelgiji.
Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia

Akizungumza
bungeni Dodoma leo, Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo,
Juma Mkamia, wakati akijibu hoja za wabunge baada ya kusoma makadirio na
matumizi wa wizara hiyo, alisema tayari serikali imeliagiza baraza la
sanaa taifa BASATA kufanya naye mahojiano.
Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia
“Tumemtaka
ajieleze kupitia BASATA, akishajieleza serikali itachukua hatua na
niombe mheshimiwa spika kupitia bunge lako tufuku, kuliomba radhi kwa
upande wa serikali kwa kitendo kilichofanywa na mwanamuziki yule. Sio
maadili yetu na nimesema akishajieleza serikali itachukua hatua yake,” alisema Juma Mkamia.
ISHU YA SHILOLE YAZIDI KUFIKA PABAYA,,, SOMA HAPA KUPATA UNDANI.
Post a Comment