Kufichwa ukweli wa ufahamu, utambuzi na ung’amuzi wa mambo
muhimu katika maisha ndiyo msingi wa umaskini na matatizo yasiyopatiwa
ufumbuzi.
Tunu hizo muhimu hujengwa na mifumo asili ya uumbwaji wa mwanadamu ambayo ni mila na utamaduni.
Elimu sahihi ni ile inayosaidia kukuza michepuo ya
akili ambayo tayari binadamu amezaliwa nayo na hujengwa na mila,
desturi na jadi.
Kwa bahati mbaya, tunafanya juhudi kubwa kuwekeza
kwenye elimu bandia inayokaririsha watu nadharia bila kugusa michepuo ya
akili.
Elimu ya vitabu na maandiko ya watu wa kale ambayo
hayana muunganiko wala mafungamano na ujuzi wa au stadi za kufanikiwa
kimaisha ndiyo masomo ya watoto wetu sasa.
Tunafundisha masomo badala ya ujuzi na maarifa. Tunawafundisha kushindwa kufikiri na kushindwa maisha.
Kubwa zaidi, utamaduni dhaifu wa wageni ndio unaochukuliwa kwa sasa kama elimu.
Mtu akizungumza, akicheza na kuvaa kama mzungu
anashangiliwa na kupongezwa kuwa ameelimika hata kama hawezi hata
kushona kifungo cha shati lake.
Tuna maprofesa waliosomea uhandisi wa maji,
wanazungumza Kiingereza kizuri na kuvaa suti kama wazungu, lakini
nyumbani wanashindwa kuvuna maji ya mvua.
Viashiria bainifu vya elimu sahihi inayokuza
vipawa na michepuo ya akili ni kuwa na watu wanaojitambua, wanaovumbua
majibu ya matatizo yao, wanaobuni, wanaochangamkia fursa na kuwa na dira
na malengo sahihi ya maisha.
Kufahamu upo duniani kwa ajili ya nini, ili ufanye nini, kwa manufaa ya nani na wakati gani. Ndiyo nguvu ya elimu sahihi.
Tofauti na elimu bandia ambayo inakaririsha nadharia ombwe kwa watu na kuviza vipaji vyao
Post a Comment